Hapo mwanzo, jua lilikuwa mali ya jogoo. Siku moja mungu alimwomba jogoo ampe jua, lakini jogoo alikataa. Kisha mungu akawaita wanyama wote aliowaumba na akawaahidi zawadi kubwa kama wangelichukua jua kutoka kwa jogoo na kumpa yeye.
Kindi aliposikia hayo, alikwenda akajenga urafiki na jogoo ili kwa njia fulani isiyo ya haki alichukue jua kutoka kwa jogoo; lakini alishindwa katika jaribio lake. Kisha mjusi akaenda na kumwambia jogoo ajenge ua kuzunguka jua ili liwe salama, kwa kuwa wengi walikuwa wakilitamani.
Jogoo akafanya hivyo, na mjusi akapata nafasi ya kuingia ndani kwa kupanda juu ya ukuta, na hivyo akalichukua jua na kumpelekea mungu. Kisha mungu akamwambia kwamba anasikitika hakuwa na nywele zaidi za kumpa, lakini mjusi atakaa pamoja na binadamu ndani ya nyumba zao. Hii ndiyo sababu mjusi huishi ndani ya nyumba za watu.
Na kila jogoo anapowika, daima humwomba mungu amrudishie jua lake.
.png?ngsw-bypass=1)