Ananse aliendelea kumhadaa Chui, na Chui alitaka kulipiza kisasi!
"Njoo tule kifungua kinywa pamoja,"
Chui akamwambia Ananse, na akamlisha Ananse nyama nyingi.
"Umeipataje nyama yote hiyo?" Ananse akauliza.
"Ni rahisi!" akasema Chui. "Ninaenda mahali ng'ombe walipo.
Ng'ombe akilala chini,
ninaingiza mkono wangu ndani na kushika matumbo ya ng'ombe.
Kisha ninayavuta nje. Lazima uvute kwa nguvu, na usiachilie."
Ananse akafanya kama Chui alivyosema,
lakini ng'ombe akakimbia na kumburuta Ananse juu ya miamba.
Ndiyo sababu tumbo la Ananse ni jeupe:
ngozi yake ilichunika kwa miamba!
