Ananse na Simbamarara walikwenda kuwinda.
Simbamarara alikamata mbuzi, lakini Ananse hakukamata chochote.
Ananse hakupenda hilo, kwa hiyo akaamua kumhadaa Simbamarara.
"Ni mbuzi mzuri huyo!" akasema Ananse.
"Nitampeleka mbuzi huyu nyumbani, nimchinje na nimpike," akasema Simbamarara.
"Umeshasali sala ya shukrani?" Ananse akamuuliza.
Simbamarara akaona aibu. "Hapana, Ananse, bado sijasali sala ya shukrani."
"Afadhali usali sala ya shukrani sasa hivi!" akasema Ananse.
"Unganisha mikono yako useme: Asante Bwana."
Simbamarara alipounganisha mikono yake, mbuzi akajinasua na kukimbia.
Simbamarara akabaki bila chochote.
Ananse akacheka tu!
