Simbamarara alikuja kumwona Ananse.
"Nyakati ngumu!" akasema Ananse. "Hakuna chakula hapa."
Simbamarara akaondoka.
Kisha Simbamarara akamsikia mke wa Ananse akiita kwa sauti, "Chakula cha jioni kiko tayari."
Simbamarara akarudi. "Nilisheni!" akanguruma.
"Nitakugawia chakula," akasema Ananse, "ukifanya ninachokwambia."
"Sawa," akasema Simbamarara.
Ananse akaingia ndani ya chungu. "Funika mfuniko. Nikibisha, nitoe nje."
Simbamarara akafunika mfuniko. Ananse akabisha. Simbamarara akamtoa nje.
"Sasa wewe!" akasema Ananse.
Simbamarara akaingia. Ananse akafunika mfuniko.
Simbamarara akabisha, lakini Ananse hakumtoa nje.
"Nimekupata sasa!"
Ananse akampika Simbamarara na kumla.
