Ananse alimsikia Simbamarara akinguruma.
Akatazama huku na huko.
Pale alikuwa Simbamarara, amenaswa ndani ya shimo refu!
Simbamarara alikuwa akiruka na kurukaruka, akijaribu kutoroka.
Ananse akatazama chini na kutabasamu.
“Hujambo, Simbamarara!” akasema. “Una shida huko chini?”
Hilo likamkasirisha Simbamarara! Inchi kwa inchi, akaanza kujikwangua akipanda juu ya shimo.
“Unaweza, Simbamarara!” Ananse akapiga kelele. “Endelea! Endelea!”
Karibu na juu, Simbamarara akahema, “Sina… nguvu… tena…”
“Omba tu!” akasema Ananse. “Unganisha miguu yako uombe nguvu.”
Na Simbamarara alipounganisha miguu yake, akateleza hadi chini kabisa tena.
Ananse akakimbia, akicheka.
