Ananse alifika mapema kwenye karamu ya harusi ya Bwana Paka na Bi Paka.
"Nitashughulikia chakula,"
akasema Ananse. "Niachieni mimi!"
Lakini bibi na bwana harusi waliporudi kutoka harusini,
walikuta keki ya harusi imetoweka,
na divai yote imekwisha pia.
"Wewe ndiye uliyefanya hivi, Mbwa!" wakapiga kelele Paka.
Mbwa akakana.
Inzi akaenda kumtafuta Ananse na akamkuta akitembea kurudi nyumbani,
uso wake umejaa makombo ya keki.
"Wewe ndiye mwizi!" akapiga kelele Inzi.
Ananse akammeza Inzi ili anyamaze.
Tangu siku hiyo Paka na Mbwa si marafiki tena;
Inzi na Buibui ni maadui pia.
.jpeg?ngsw-bypass=1)