Tacoomah alimtembelea Ananse.
Ananse alikuwa na mayai mia moja kwenye kiota,
na Tacoomah mroho akala mayai tisini na tisa ya Ananse.
Kisha Ananse akasema,
"Nitahesabu mayai yangu!"
"Huna haja," akasema Tacoomah.
"Nitakuhesabia mimi."
"Inua kila yai juu ili nilione,"
akasema Ananse.
Tacoomah akatoka nje kwenye kiota na
akainua yai moja ili Ananse aweze kuliona.
"Moja!" akasema Tacoomah.
Kisha Tacoomah akalishusha yai kwenye kiota na
akaliinua yai lilelile tena. "Mbili!" akasema.
Basi Tacoomah akafanya hivyo mara mia moja...
lakini kulikuwa na yai moja tu.
.jpeg?ngsw-bypass=1)