Moto wa Ananse ulizimika.
"Mwanangu," akasema Ananse,
"nenda kwa Tacoomah ukaombe moto."
Tacoomah akampa mtoto moto kidogo.
"Chukua na mafuta haya ya ng'ombe pia!" akasema Tacoomah.
Mtoto akarudi na moto na mafuta ya ng'ombe.
"Hicho kitu kichafu ni nini?" Ananse akauliza.
"Tacoomah amenipa."
"Aah!" akasema Ananse.
"Nitakitupa."
Ananse alikuwa akijifanya tu;
aliyala mafuta ya ng'ombe na akataka zaidi.
Ananse akaumwagia moto maji.
"Nenda ukaombe moto zaidi!" akamwambia mtoto wake mwingine.
Mtoto akarudi na moto na mafuta ya ng'ombe.
Ananse akafanya hila ileile na akayala mafuta ya ng'ombe,
huku watoto wake wakilala njaa.
.jpeg?ngsw-bypass=1)