Ananse na Tacoomah walikuwa wakimchumbia mwanamke mmoja.
Tacoomah akamwambia,
"Ananse alikuwa farasi wa kupanda wa baba yangu!"
Ananse aliposikia hayo alikasirika.
"Twende tukamwambie ukweli!" akasema Ananse.
"Siwezi kwenda sasa," akasema Tacoomah. "Ninaumwa."
"Lazima twende sasa hivi!" akasema Ananse.
"Basi," akasema Tacoomah, "labda unaweza kunibeba."
Ananse akamwacha Tacoomah apande mgongoni mwake.
"Nimedhoofika mno..." akasema Tacoomah.
"Nahitaji fimbo yangu ya kutembelea ili nijishikilie."
Walipokaribia nyumba ya yule mwanamke,
Tacoomah akaanza kumchapa Ananse kwa fimbo ya kutembelea.
Ananse akakimbia.
"Tazama!" Tacoomah akapiga kelele.
"Ananse alikuwa farasi wa kupanda wa baba yangu, na sasa ni wangu!"
.jpeg?ngsw-bypass=1)