Fisi alitakiwa kumtupa Mjanja-Kuliko-Baba baharini,
lakini Mjanja-Kuliko-Baba alirudi nyumbani,
na akaleta kundi la kondoo pamoja naye.
"Lakini nilimtupa baharini!" Fisi akapiga kelele.
"Ndiyo, ulinitupa!" akasema Mjanja-Kuliko-Baba.
"Hawa ni kondoo wa baharini, na pale bahari inapokuwa na kina zaidi,
kondoo ni wakubwa zaidi."
"Nataka kondoo wakubwa!" akapiga kelele Ananse.
"Fisi, niweke ndani ya jeneza unitupe kwenye bahari yenye kina kirefu kuliko zote."
Ananse akaingia ndani ya jeneza na
Fisi akakodi mashua kusafiri hadi bahari yenye kina kirefu kuliko zote.
Akalitupa jeneza majini.
Huo ukawa mwisho wa Ananse.
.jpeg?ngsw-bypass=1)