Ananse alimchukia mwanawe Mjanja-Kuliko-Baba na alitaka kumuua.
Wakati Ananse akipanga njama na Fisi,
Mjanja-Kuliko-Baba alijifanya amelala chini ya meza,
lakini alikuwa akisikiliza.
"Nisaidie kumuua!" Ananse akamwambia Fisi.
"Nitajificha kwenye mche wa pilipili," akasema Fisi. "Mtume mwanao huko."
Wakati wa chakula cha jioni, Ananse akasema, "Mwanangu, nenda ukachume pilipili kwenye mche wa pilipili!"
Lakini Mjanja-Kuliko-Baba akachukua kijiti kutoka motoni na akauchokoa mche wa pilipili.
Kijiti cha moto kikamchoma Fisi usoni! Fisi akapiga yowe na kukimbia.
Kisha Mjanja-Kuliko-Baba akamwambia Ananse,
"Mche wa pilipili ulipiga yowe,
kwa hiyo sikuchuma pilipili yoyote."
Ananse alilazimika kula chakula cha jioni bila pilipili.
.jpeg?ngsw-bypass=1)