Ananse alipanda kiazi kikuu maalumu kilichoitwa kiazi-fufu,
na kikakua kikubwa!
Akapeleka kiasi nyumbani na akakipika.
"Niambieni jina la kiazi hiki,"
akasema Ananse. "La sivyo, hamtakula."
Hakuna aliyejua jina la kiazi hicho,
kwa hiyo Ananse akakila kiazi chote.
Siku iliyofuata, mwana mdogo kabisa wa Ananse,
Mjanja-Kuliko-Baba,
akaponda bamia kadhaa na akazitandaza ardhini.
Kisha akajificha na kutazama.
Akirudi nyumbani,
Ananse akateleza juu ya bamia na akaanguka.
"Ole wangu! Nimeangusha kiazi-fufu changu!" akapiga kelele.
Mjanja-Kuliko-Baba akakimbia nyumbani na akamwambia kila mtu.
Ananse alipokipika kiazi,
mkewe na watoto wake wakasema,
"Tupe kiazi-fufu!" na Ananse akalazimika kugawana nao.
.jpeg?ngsw-bypass=1)