Mke wa Ananse alifuga nguruwe.
"Tumle nguruwe wako!" akasema Ananse.
"Hapana!" akasema. "Nitamuuza."
Kisha Ananse akajifanya anaumwa.
"Mlete daktari," akaugua.
Mara tu alipoondoka,
Ananse akajivisha kama daktari
na akakimbia kumkuta njiani.
"Nina shughuli nyingi mno siwezi kutembelea wagonjwa nyumbani,"
akasema, "lakini mchuzi wa nyama ya nguruwe ni dawa nzuri."
Mke wa Ananse akaelekea nyumbani,
na Ananse akakimbia ili afike kwanza.
"Daktari anasema lazima ule mchuzi wa nyama ya nguruwe,"
akasema mke wa Ananse.
"Ninaumwa mno siwezi kula..."
Ananse akalalamika.
"Lazima ule mchuzi wa nyama ya nguruwe,"
akajibu. "Ni agizo la daktari!"
Ananse akatabasamu.
.jpeg?ngsw-bypass=1)