Ananse na familia yake walikuwa wakifa njaa.
Mwishowe, Ananse akapata chakula: ndizi za kupika.
Kulikuwa na ndizi nne, lakini midomo mitano ya kulisha: Ananse,
Bi Ananse, wavulana wawili na binti mmoja.
Bi Ananse akazichoma ndizi,
na Ananse akampa kila mtoto moja na mkewe moja.
"Msijali kuhusu mimi," akasema kwa huzuni.
"Wewe huna njaa?" akauliza binti yake.
"Ninakufa njaa, mwanangu mpendwa," akasema Ananse. "Lakini usijali."
Akaivunja ndizi yake na akampa Ananse nusu.
Wavulana wawili wakafanya hivyo hivyo.
Na Bi Ananse pia.
Kwa hiyo Ananse akaishia kuwa na chakula kingi kuliko mtu yeyote.
