Ananse aliiba ndizi kutoka kwenye mgomba wa Mbuzi.
"Meee-e-e, ndizi zangu ziko wapi?"
akapiga kelele Mbuzi. Mbuzi akakimbia nyumbani kwa Ananse.
Ananse na familia yake wakajificha juu ya paa.
Mtoto mmoja akateleza akaanguka. Mbuzi akamdaka mtoto,
akamuua, na akamtia ndani ya gunia.
"Meee-e-e, sasa yeye ndiye ndizi yangu!"
Mmoja baada ya mwingine watoto wote wakateleza.
Kisha Bi Ananse akateleza.
"Meee-e-e, sasa wote ni ndizi zangu!" akasema Mbuzi.
"Wewe ndiye unayefuata, Ananse!"
"Tengeneza lundo la majivu nianguke juu yake," akasema Ananse.
"Kisha nitateleza." Mbuzi akakusanya majivu.
Ananse akaanguka. Majivu yakatawanyika kila mahali!
Mbuzi hakuweza kuona, na Ananse akatoroka.
.jpeg?ngsw-bypass=1)