Simba alijifanya amekufa barabarani.
Ananse akamkuta na akambeba hadi nyumbani ili amle.
"Tazama hiki!" Ananse akapiga kelele.
"Simba amekufa!"
Mke wa Ananse akautikisa mkia wa Simba;
Simba akatetemeka. "Simba hajafa!"
akapiga kelele. "Ndiyo, amekufa!" akapiga kelele Ananse.
Kisha, mke wa Ananse akavuta kucha la Simba.
"Simba hajafa!" akapiga kelele.
"Ndiyo, amekufa!" Ananse akapiga kelele.
Kisha mke wa Ananse akaona kwamba macho ya Simba yalikuwa wazi.
"Simba hajafa!" akapiga kelele.
"NGRAAA!" akanguruma Simba. "KIMBIA!" akapiga kelele Ananse.
Wakakimbilia kwenye mihimili ya paa. Mke wa Ananse akaanguka;
Simba akamla.
Ananse akaruka nje kupitia dirishani na akaichoma nyumba moto
… Simba akiwa ndani!
.jpeg?ngsw-bypass=1)