Ananse na Simba walinunua mahitaji mjini.
Walipokaribia kufika nyumbani Ananse akasema,
"Nimesahau sharubati ya miwa! Wewe rudi ukaichukue.
Mimi nitaendesha mkokoteni hadi nyumbani!" Simba alipoondoka,
Ananse akaficha mkokoteni na punda vichakani.
Kisha, akakata mkia wa punda.
Halafu akaufukia mkia ukiwa umesimama wima
nje ya ardhi. Simba aliporudi,
Ananse akapiga kelele,
"Punda amekimbilia chini ya ardhi!
Kamata mkia kabla hajatoroka!"
Simba akaushika mkia na kuuvuta.
"Ole wangu! Nimeung'oa mkia wa punda!"
Simba akalalamika.
"Sasa hatutaupata tena mkokoteni kamwe."
.jpeg?ngsw-bypass=1)