Ananse aliingiza mkono wake ndani ya shimo.
Shimo likasema,
"Mimi ni Kurusha-Maili!"
Kisha likamrusha Ananse umbali wa maili moja.
"Safi sana!" akasema Ananse,
na akasimika vigingi vikali pale alipoangukia.
Kisha Ananse akamwongoza Nguruwe hadi kwenye shimo.
"Ingiza mkono wako!" akasema Ananse.
Kurusha-Maili likamrusha Nguruwe;
Nguruwe akatobolewa na kigingi.
"Nitamla Nguruwe baadaye!" akasema Ananse,
kwa furaha. Kisha Mbuzi. Kisha Mbwa.
Tumbili akatazama alichokuwa akifanya Ananse.
Kisha Ananse akamwongoza Tumbili hadi kwenye shimo.
"Tazama!" Tumbili akapiga kelele.
"Kuna dhahabu ndani ya shimo!"
Ananse mroho akanyoosha mkono kuchukua dhahabu.
Kurusha-Maili likamrusha Ananse
na akatobolewa na kigingi.
Tumbili akacheka.
.jpeg?ngsw-bypass=1)