Zamani Tumbili alikuwa maridadi na mstaarabu.
Maneno ya kifahari. Adabu za hali ya juu.
Wanyama wote walimheshimu Tumbili kwa umaridadi wake.
Hilo likamfanya Ananse aone wivu,
kwa hiyo Ananse akapata suti ya kifahari na akaijaza sisimizi.
"Ee, Tumbili!" Ananse akapiga kelele.
"Wewe unajua kila kitu kuhusu mitindo ya kifahari.
Suti hii itanipendeza?"
"Suti nzuri ilioje!" akasema Tumbili.
"Nitafurahi kukuvalia ili uione, Ananse."
Tumbili akavaa suti,
na mara moja akaanza kutetemeka na kujikuna,
akirukaruka juu na chini, akigaagaa chini.
Sisimizi walikuwa wakimuuma Tumbili mwili mzima!
Na tangu siku hiyo Tumbili amekuwa akifanya mambo ya kipumbavu.
.jpeg?ngsw-bypass=1)