Ananse alikuwa na deni la pesa kwa Tumbili,
lakini hakuweza kulipa,
kwa hiyo Tumbili akamchapa Ananse mjeledi.
Siku iliyofuata Tumbili akaja akamchapa Ananse tena.
Ananse akamwambia mama yake,
"Washa moto, uniweke ndani ya chungu,
na unifiche ndani ya majivu."
Lakini Tumbili alikuwa mchawi aliyeona vitu vilivyofichwa,
na akamkuta Ananse ndani ya majivu.
Akamchapa Ananse tena.
Mchawi mwingine akampa Ananse kamba ya uchawi.
Ananse akapanda kamba ya uchawi.
Tumbili akapanda kamba nyuma yake.
Ananse akapiga kelele, "Kamba: katika!"
Tumbili akaanguka chini akavunjika shingo.
Kisha Ananse akapiga kelele, "Kamba: ungana!"
na akashuka salama.
.jpeg?ngsw-bypass=1)