Ananse na Fisi walikwenda mtoni.
"Toa matumbo yako kabla ya kuoga!"
Ananse akamwambia Fisi, na Fisi akafanya hivyo.
Kisha Ananse akala matumbo ya Fisi wakati Fisi akioga.
"Matumbo yangu yako wapi?" akapiga kelele Fisi.
"Tumbili wameyapeleka matumbo yako Mji wa Tumbili,"
akasema Ananse. Fisi akakimbia hadi Mji wa Tumbili,
na tumbili wote walikuwa wakiimba:
"Tumbili wote tumeyameza!
Tumekula matumbo ya Bwana Fisi!"
Fisi akakasirika na akaanza kuwaua tumbili.
Mmoja wa tumbili akapiga kelele,
"Acha hivyo, Fisi! Ni wimbo tu!
Ananse alitufundisha wimbo huu jana."
Basi Fisi akajua kwamba Ananse alikuwa amemhadaa tena.
.jpeg?ngsw-bypass=1)