"Hicho ni nini?" Fisi akamuuliza.
"Mkojo wa Tumbili!" akasema Ananse, akitabasamu.
"Onja!" Fisi akaonja asali.
"Mkojo wa Tumbili ni mtamu!" Fisi akakimbia kumkamata Tumbili,
na Ananse akaenda pamoja naye kutazama.
Fisi akamshika Tumbili shingoni kwa mkono mmoja,
na akanyoosha mkono wake mwingine.
"Kojoa mkononi mwangu!" Fisi akamnguruma Tumbili.
Tumbili akatii, na Fisi akanywa mkojo.
"Aah! Huu si mtamu hata kidogo!"
Ananse akampigia Fisi kelele.
"Usimkamate kwa nguvu hivyo! Legeza mshiko wako,
na mkojo wa Tumbili utakuwa mtamu."
Fisi akalegeza mshiko wake, na Tumbili akakimbia.
Ananse akacheka tu.
.jpeg?ngsw-bypass=1)