"Hadithi zote zitakuwa zako ukiniletea nyuki ndani ya kibuyu,"
Fisi akamwambia Ananse.
Ananse akachukua kibuyu na akaingia msituni, akinung'unika.
Malkia wa Nyuki akauliza, "Kuna nini, Ananse?"
"Nimewekeana dau na Fisi kuhusu idadi ya nyuki kibuyu hiki kinachoweza kubeba,"
akasema Ananse. "Lakini sijui jibu."
"Hata mimi sijui!" akasema Malkia wa Nyuki.
"Tutafute jibu. Unaweza kutuhesabu!"
Kisha nyuki wakamfuata malkia wao,
wakivuma vuuu-vuuu-vuuu kuingia ndani ya kibuyu cha Ananse.
Kibuyu kilipojaa,
Ananse akaziba tundu na akampelekea Fisi kibuyu.
"Sasa hadithi zote ni zangu!" Ananse akapiga kelele.
.jpeg?ngsw-bypass=1)