"Hadithi zote zitakuwa zako ukiniletea mavu ndani ya kibuyu,"
Fisi akamwambia Ananse.
Ananse alijua hasa la kufanya.
Akatoboa tundu kwenye kibuyu.
Akajaza bakuli maji.
Kisha akapata kundi la mavu na akawamwagia maji.
Akiwa ameshika bakuli juu ya kichwa chake kama mwavuli,
Ananse akapiga kelele,
"Mvua inanyesha! Wajinga pekee ndio hukaa nje mvuani.
Njooni mjifiche ndani ya kibuyu hiki kizuri kikavu."
Mavu walipokwisha kuingia ndani ya kibuyu,
Ananse akaziba tundu na akampelekea Fisi kibuyu.
"Sasa hadithi zote ni zangu!"
Ananse akapiga kelele.
.jpeg?ngsw-bypass=1)