Ruka hadi maudhui makuu
Folktale

Jinsi Ananse Alivyoshinda Hadithi Zote: Hadithi ya Nyoka Aliyepimwa — Hadithi ya Jadi ya Afrika Magharibi

1 dakika za kusoma

African Folklore illustration – Jinsi Ananse Alivyoshinda Hadithi Zote: Hadithi ya Nyoka Aliyepimwa — Hadithi ya Jadi ya Afrika Magharibi

Sikiliza hadithi hii

Bofya kupakia kicheza sauti

Spotify

Hadithi zote zitakuwa zako ukiweza kumkamata Nyoka akiwa hai na kumleta hapa,"

Fisi akamwambia Ananse.

Basi Ananse akaenda kumwona Nyoka.

Akamkodolea Nyoka macho hadi Nyoka akauliza,

"Unakodolea macho nini?"

"Fisi alisema wewe si mrefu kama fimbo hii!"

Ananse akampungia Nyoka fimbo.

"Lakini mimi nilisema wewe ni mrefu kuliko.

Wewe ndiye mnyama mrefu kuliko wote,

kwa hiyo lazima uwe mrefu kuliko fimbo hii."

"Ndiyooooo!" akasema Nyoka.

"Nitakuonyesha!"

Nyoka akajinyoosha kando ya fimbo.

Kisha Ananse akamfunga Nyoka kwa nguvu na akampeleka kwa Fisi.

"Sasa hadithi zote ni zangu!"

Ananse akapiga kelele.