Mfalme Fisi alikuwa na kigoda kimoja cha dhahabu na vigoda vinne vya fedha.
Yeyote ambaye angehesabu vigoda vyote angeanguka na kufa,
lakini wanyama hawakujua hilo.
"Shinda kigoda cha dhahabu!" akasema Fisi.
"Hesabu tu vigoda vingine.
Hilo tu ndilo unalohitaji kufanya!" Paka akaja akahesabu:
"Moja, mbili, tatu, nne, tano." Paka akaanguka na kufa.
Fisi akamla. Kisha Sungura, Mbwa, Tumbili, ikawa vilevile.
Ananse akaja. "Moja, mbili, tatu, nne,"
akasema Ananse, "na kimoja zaidi!" Fisi akakasirika.
"Hivyo sivyo mtu anavyohesabu!" akapiga kelele.
"Hivi ndivyo unavyohesabu: Moja, mbili, tatu, nne, tano!"
Fisi akaanguka na kufa.
