Simbamarara, Ananse na Mbuzi waliishi pamoja katika nyumba moja,
lakini Simbamarara alitaka nyumba yote iwe yake peke yake.
"Nina njaa!" Simbamarara akanguruma.
"Nitawala nyote wawili!"
Kisha Ananse na Mbuzi wakakimbia, na Simbamarara akawafukuza.
Wakafika mtoni.
"Siwezi kuogelea!" akalia Mbuzi.
Ananse akamgeuza Mbuzi kuwa jiwe dogo jeupe,
kisha Ananse akaruka kuvuka mto.
Simbamarara akafika.
"Nakuwekea dau huwezi kunipiga kwa jiwe hilo!"
Ananse akampigia kelele Simbamarara.
Simbamarara akalirusha jiwe. Lilipogusa ardhi upande wa pili,
jiwe likageuka tena kuwa Mbuzi. Ananse na Mbuzi wakawa salama!
