Ananse na Simbamarara walitaka kuona mkono wa nani una nguvu zaidi.
Ananse akaficha nyundo ndani ya mkono wa shati lake na akampiga Simbamarara kichwani.
Simbamarara alishangaa.
Hakujua kwamba mkono wa Ananse ulikuwa na nguvu hivyo.
"Nitakuja kukupiga kesho!" akasema Simbamarara.
Basi Ananse akamwalika Paa nyumbani kwake.
"Nitapumzika kidogo sasa," akasema Ananse,
"lakini Simbamarara ananiletea chakula kizuri cha jioni!
Akibisha hodi, mkaribishe ndani."
Simbamarara akabisha hodi, na Paa akafungua mlango.
Simbamarara akampiga na kukimbia, akidhani amempiga Ananse.
Paa alikuwa amekufa, kwa hiyo Ananse akamchoma Paa na kumla.
