Simbamarara alitaka kumuua Ananse.
"Mwambie nimekufa,"
Simbamarara akamwambia Bi Simbamarara.
"Nitalala hapa nimsubiri."
Bi Simbamarara akapiga kelele, "Maskini Simbamarara!
Bwana Simbamarara amekufa!" Ananse akaingiwa na shaka.
"Ulisikia kwamba Simbamarara alikuwa anaumwa?" akamuuliza Mbwa.
Mbwa akasema hapana.
Akamuuliza Tumbili na Mbuzi na wanyama wote.
Hakuna aliyesikia kwamba Simbamarara alikuwa anaumwa.
Ananse akaenda nyumbani kwa Simbamarara.
Bi Simbamarara alikaa pale akilia, na
Simbamarara alikuwa kitandani. "Ameshatoa mguno wa mwisho?"
Ananse akamuuliza Bi Simbamarara.
"Wafu hutoa mguno mkubwa wa mwisho."
Simbamarara akaguna. K
isha Ananse akakimbia, akicheka.
