Simbamarara na Ananse walikwenda mtoni.
"Osha matumbo yako!" Ananse akamwambia Simbamarara.
Simbamarara akatoa matumbo yake na akayaosha.
"Sasa kichwa chako!" Simbamarara alipotumbukiza kichwa chake majini,
Ananse akaiba matumbo ya Simbamarara. "Pika mchuzi kwa haya!"
Ananse akamwambia mkewe.
Kisha Ananse akawaandaa watoto wake kwa ajili ya mazishi ya Simbamarara.
"Kila mtu apige kelele: Maskini Simbamarara amekufa!" Mtoto mmoja akalia,
"Tulimla Simbamarara!" "Hapana!" akasema Ananse.
"Wewe huwezi kwenda mazishini."
Lakini mtoto huyo akaenda mazishini hata hivyo.
Ananse alipomwona mtoto akija,
akakimbia akajificha juu ya paa.
Buibui hukaa juu ya paa hadi leo.
