Ananse alikuwa amebeba kikapu cha samaki alipokutana na Simbamarara.
Simbamarara akanyakua kikapu na akala samaki.
Ananse alikasirika lakini hakusema neno.
Wakaendelea kutembea. Ananse akaona mti wa matunda.
"Kuna matunda mazuri pale!" akasema Ananse.
"Niletee baadhi!" akasema Simbamarara.
Ananse akapanda juu na akatazama chini.
"Naona chawa kwenye manyoya yako!" Simbamarara akasema,
"Nisafishe!" Ananse akashuka na akavuta
manyoya na sharubu za Simbamarara, na kwa manyoya na sharubu za Simbamarara
akamfunga Simbamarara kwenye mti!
Kisha Ananse akakimbia na kumwacha Simbamarara amefungwa kwenye mti.
Simbamarara akanguruma, na mwindaji akaja na kumuua.
