Ananse na Simbamarara walikwenda kuvua samaki.
Walipovua samaki mmoja, Simbamarara akamnyakua.
"Huyu ni wangu!" akapiga kelele.
Simbamarara akamfunga samaki kwa uzi kisha akaufunga uzi huo kwenye kidole chake cha mguu.
"Nikitikisa kidole changu, nitajua samaki yupo."
Kisha Simbamarara akalala,
akitikisa kidole chake kuhakikisha samaki yupo.
Ananse akamfungua samaki kwa uangalifu na akaufunga uzi kwenye mti.
Simbamarara aliendelea kutikisa kidole chake, akidhani samaki yupo.
Simbamarara alipoamka, akavuta uzi.
Hakuna samaki! Hapo Simbamarara akajua kwamba Ananse amemhadaa.
