Chui na Ananse waliwinda nguruwe wa Bwana Mtu.
Kila mara Chui alipofyatua risasi, Ananse naye alifyatua.
Chui aliwapiga nguruwe.
Ananse hakupiga chochote, lakini bado alidai nusu ya nyama.
Hilo likamkasirisha Chui, kwa hiyo akafanya hila. "Namsikia Bwana Mtu anakuja!" Chui akapiga kelele.
Wote wawili wakajificha.
PAA! Chui akatoa sauti ya mjeledi. PAA! Chui akatoa sauti hiyo tena.
"Nani amewapiga risasi nguruwe wangu?" akasema Chui kwa sauti ya Bwana Mtu.
"Chui ndiye aliyewapiga nguruwe!" Ananse akapiga kelele.
PAA!
"Si mimi, Bwana Mtu! Mimi sijui kupiga risasi! Chui ndiye aliyewapiga nguruwe hao."
Chui akamcheka Ananse na akapeleka nyama yote nyumbani.
Ananse hakupata chochote.
